Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mkutano wa Darfur kuhusu maji kuandaliwa Khartoum

Mkutano wa Darfur kuhusu maji kuandaliwa Khartoum

Mkutano mkuu wa kimataifa kuhusu maji kwenye jimbo la Darfur unatarajiwa kuandaliwa tarehe 12 mwezi Aprili mwaka huu kwenye mji mkuu wa Sudan Khartoum.

Kuna uhaba mkubwa wa mvua kwenye jimbo la Darfur na hiyo ndiyo inaonekana kama sababu kuu inayosababisha mizozo kati ya jamii za wavugaji zinazotafuta lishe kwenye ardhi ya wakulima mimea. Lengo la kwanza la mkutano huo litakuwa ni kutoa hamasisho kuhusu matatizo ya uhaba wa maji kwa watu wa Darfur. Lengo la pili la mkutano huo ni kuchangisha fedha zitakazotumia kufadhili miradi zaidi ya maji kwenye jimbo la Darfur. Pia fedha zitakazopatikana zitatumika katika kuwahakikishia walihama makwao mazingira mema ili wapate kurejea nyumbani. Serikali ya Sudan iko kwenye mstari wa mbele kwa ushirikiana na Umoja wa Mataifa na UNAMID kuufanikisha mkutano huo. Emmanual Mollel mkuu wa kitengo cha cha utunzi wa mazingira katika kikosi cha UNAMID anaeleza:

(SAUTI YA EMMANUEL MOLLEL)