Ban atoa wito wa mabadiliko nchini Misri:

Ban atoa wito wa mabadiliko nchini Misri:

Nchini Misri waandamanaji wanaopinga serikali wameendelea na maandamano kwenye uwanja wa Tahrir. Wanataka Rais Hosni Mubaraka ajiuzulu mara moja.

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amekuwa akitoa wito kwa serikali ya nchi hiyo kusikiliza matakwa ya watu na kuchukua hatua zinazofaa kwa kituo na kwa amani.

(SAUTI YA BAN KI-MOON)

Pia amelaani ghasia na vitisho dhidi ya waandamanaji, pia waandishi wanaoripoti habari za yanayotokea Misri. Amesema ghasia na vitisho lazima vikome sasa na hasa vikwazo dhidi ya vyombo vya habari vya kimataifa, waandishi wa habari na wanaharakati wa haki za binadamu, kwani ni jambo lisilokubalika.

Ban yuko Ujerumani ambako amekutana na cancela wa nchi hiyo bi Angela Merkel kujadili mabadiliko kwenye Umoja wa Mataifa, mabadiliko ya hali ya hewa na upokonyaji wa silaha miongoni mwa mengi wanayojadili. Pia anahudhuria mkutano wa masuala ya usalama mjini Munich .