Skip to main content

Ghasia za Misri zatoa onyo kwa usalama wa chakula:UM

Ghasia za Misri zatoa onyo kwa usalama wa chakula:UM

Mkurugenzi wa shirika la mpango wa chakula duniani WFP Josette Sheeran amesema kuwa yale yanayoendelea kushuhudiwa katika eneo la mashariki ya katika majuma machache yaliyopita ni onyo kuhusu umuhimu wa usalama wa chakula katika kutuliza hasira za watu.

Sheeran amesema kuwa hata kama maandamano hayo yanachochewa na sababu nyingi lakini pia waandamanaji hawa wana sababu moja ambayo ni kupanda kwa bei cha chakula. Sheeran anasema kuwa maandamano na ghasia katika eneo la mashariki ya kati yanaenda sambamba na kipindi kingine cha kupanda kwa bei ya chakula duniani.

Makadirio cha bei ya chakula ya shirika la WFP yanaonyesha kuwa mwezi Januari bei ya chakula ilipanda na kuweka historia kwa kupanda kwa mwezi wa saba mfululizo zaidi ya bei iliyoshuhudiwa mwaka 2007 na 2008.