Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UM wasikitishwa na serikali ya mpito Somalia kujiongezea muda

UM wasikitishwa na serikali ya mpito Somalia kujiongezea muda

Mwakilishi maalumu wa katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa nchini Somali Balozi Augustine Mahiga ameelezea kuhuzunishwa kwake na hatua ya serikali ya mpitio ya Somali ya kuongeza muda wake wa kuhudumu kwa miaka mitatu .

Mahiga amesema kuwa hatua hii ilichukuliwa bila ya kupata ushauri jinsi ya kukamilisha muda uliowekwa wa kuhudumu kwa serikali ya mpito ya Somali mnamo tarehe 20 mwezi Agosti mwaka huu.

Mahiga anasema kuwa watu wa Somali wanatarajiwa kuona mabadiliko na kuongeza kuwa ni wajibu wa serikali ya mpito kutekeleza mabadiliko haya kwa kushirikisha pande zizowakilisha watu wa Somali na washirika wengine wa jamii ya kimataifa. Hata hivyo amesema kuwa wataendelea kushirikiana na utawala wa Somali.