UM wakarabisha matokeo ya duru ya kwanza ya uchaguzi Haiti

UM wakarabisha matokeo ya duru ya kwanza ya uchaguzi Haiti

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon na mwakilishi wake maalumu nchini Haiti Edmond Mulet, wamekaribisha tangazo rasmi la baraza la uchaguzi la Haiti la matokeo rasmi na ya mwisho ya uchaguzi wa duru ya kwanza wa bunge na Rais.

Wamesema ni muhimu kwa mchakato wa uchaguzi kuendelea kufuatia miwezi zaidi ya miwili ya sintofahamu kwa Wahaiti.

Mulet amerejea hoja ya Umoja wa Mataifa kuwa tayari kulisaidia baraza la uchaguzi na serikali ya Haiti katika kuendesha mchakato wa duru ya pili ya uchaguzi na hususan kuhakikisha unafanyika vyema, wa uwazi na unaostahili.