Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Athari za kunakili kazi zajadiliwa kwenye UM:WIPO

Athari za kunakili kazi zajadiliwa kwenye UM:WIPO

Sasa ni bayana kwamba biashara haramu ya bidhaa bandia pamoja na wizi wa kunakili kazi za wengine sio tu vinasababbisha hasara ya dola trillion moja kila mwaka duniani na kuhatarisha zaidi ya nafasi za kazi milioni mbili bali pia vinahatarisha maisha na afya ya watumizi wake kote duniani.

Haya yalisemwa kwenye mkutano ulioandaliwa na Umoja wa Mataifa uliohudhuriwa na zaidi ya wajumbe 800 kutoka zaidi ya nchi 100 uliondaliwa mjini Paris nchini Ufaransa. Mkutano huo wa siku mbili ulioandaliwa kwa ushirikiano wa mashirika ya INPI , shirika la kulinda haki kumiliki biashara WIPO, polisi wa kimataifa INTERPOL na washikadau wengine ulijadili njia za kukabiliana na tatizo hilo.

Akifungua mkutano huo mkurugenzi WIPO Francis Gurry amesema kuwa huu ni wakati mwafaka kwa sekta za kibinafsi na za umma kuungana kupambana na tatizo hilo.