Skip to main content

Licha ya machafuko Somalia isisahaulike:Amos

Licha ya machafuko Somalia isisahaulike:Amos

Mratibu wa Umoja wa Mataifa wa masuala ya kibinadamu na dharura Bi Valarie Amos leo amehitimisha ziara ya siku tatu nchini Kenya na Somalia.

Katika ziara hiyo ametathimini operesheni za misaada na changamoto zinazoikabili jumuiya ya wahisani.

Wakati wa ziara hiyo Bi Amos amekutana na viongozi wa serikali wan chi zote mbili na kujadili masuala ya ongezoko la wakimbizi na masuala ya wakimbizi wa ndani ambao ni matokeo ya vita na janga la ukame.

Pia amesisitiza haja ya kupata fursa ya kuwafikia watu wenye mahitaji hasa kwenye maeneo yanayokabiliwa na vita nchini Somalia.

Ameishukuru serikali ya Kenya kwa mchango wake mkubwa wa kuhifadhi wakimbizi wa Somalia, na kwa upande wa Somalia amesema taifa hilo ambalo halina serikali imara kwa miongo miwili sasa isisahaulike.

(SAUTI YA VALARIE AMOS)