Skip to main content

Kuimarika kwa uchumi kwaongeza kasi ya wasafiri wa anga:UM

Kuimarika kwa uchumi kwaongeza kasi ya wasafiri wa anga:UM

Ripoti moja iliyotolewa na Umoja wa Mataifa inaonyesha kuwa safari za anga mwaka uliopita 2010 zilipata mafanikio makubwa ikilinganishwa na mwaka mmoja nyuma ambapo dunia ilikubwa na mkwamo wa kiuchumi.

Katika ripoti yake ya kila mwaka, shirila la Umoja wa Mataifa linaloshughulika na masuala ya usafiri wa anga ICAO, imesema kuwa kuongezeka kwa safari za anga kumetokana na kuanza kuimarika kwa hali ya uchumi baada ya kushuhudia kipinda cha mkwamo wa mwaka mmoja nyuma.

ICAO imesema kuwa kiwango cha wasafiri katika mwaka 2010 kiliongezeka kwa asilimia 6.3 huku idadi ya mizigo ikivunja rekodi ya mwaka uliopita na kupanda kwa asilimia 18.9 .

Shirika hilo la umoja wa mataifa limesema kuwa nchi za Ulaya ndizo zilizonufaika zaidi kutokana na kiwango cha chini cha gharama za usafiri wa anga.