Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mtandao wa kumbukumbu za watumwa wazinduliwa

Mtandao wa kumbukumbu za watumwa wazinduliwa

Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki -moon amepongeza kuzinduliwa kwa mtandao ya kuwakumbuka waathiriwa wa bishara ya utumwa na kuitaja kama hatua muhimu.

Kwenye ujumbe uliosomwa kwa niaba yake na naibu katibu wa masuala ya habari na mawasiano kwenye uzinduzi wa mtandao huo Kiyo Akasaka ,Ban amesema kuwa hatua hii inakumbusha wengi kuwa mamilioni ya waafrika waliondolewa kwa nguvu kutoka makwao na kudhulumiwa.

Ban amesema kuwa makumbusho hayo pia yanaukumbusha ulimwengu kuhusu ujasiri wa watumwa hao na mashujaa wengine ambao walifanikiwa kuinuka na kukomesha utumwa. Ban anasema kuwa utumwa unaendelea kuonekana hususan kupitia kwa ajira ya lazima, kuwasafirisha kiharamu wanawake na watoto , ndoa za lazima pamoja na ajira ya watoto.