Umoja wa Mataifa leo umezindua mwaka wa jukumu la mistitu
Umoja wa Mataifa leo umezindua mwaka wa kushereheakea jukumu muhimu linafanywa na misitu duniani.
Chama cha kimataifa kinachuhusika na utunzi wa mambo ya asili kimesema kuwa misitu ina umuhimu mkubwa unaoweza kufaidi serikali na jamiii zinazoishi karibu na misitu hiyo.
Kulingana na ripoti iliyotolewa na chama hicho wakati wa kuadhimishwa kwa siku ya kimataifa ya misitu kwenye makao ya Umoja wa Mataifa ni kuwa sekta za kibinafsi zinazowekeza kwenye misitu zimenufaika kwa miaka mingi na sasa huu ni wakati wa sekta za umma nazo kunufaika.
Ripoti hiyo pia inapendekeza misitu kusimamiwa na jamii zinaoishi karibu na misitu ikisema kuwa sekta ya misitu inapata ufadhili wa dola bilioni 12 kutoka kwa sekta ya umma kila mwaka huku asimilia kidogo ya fedha hizo ikielekezwa kwa sekta ya msitu inayosimamiwa na jamii.