Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Burundi iharakishe kuunda tume ya haki za binadamu:UM

Burundi iharakishe kuunda tume ya haki za binadamu:UM

Mtaalumu wa kujitegemea wa Umoja wa Mataifa Fatsah Ouguergouz amekaribisha hatua iliyochukuliwa na serikali ya Burundi kupitisha sheria inayotaka kuwepo wa kamishna huru ya taifa inayoshughulikia masuala ya haki za binadamu, lakini hata hivyo ametaka kuharakishwa mara moja uundwaji wa kamishna hiyo.

Bunge la nchi hiyo pamoja na seneti lilipitishwa mwezi wa disemba mwaka jana sheria hiyo ambayo inafungua uwanja wa kuwepo kwa kamishna ya haki za binadamu.

Mtaalamu huyo ametaka mamlaka nchini humo kuteua makamishna watakaohudumu kwenye chombo hicho kwa kuzingatia misingi ya uwazi na ukweli ili hatimaye kufanikisha utendaji wake kazi utaojumuisha makundi yote ya jamii.

Ametaka chombo hicho kisisalie kwenye makaratasi pakee, bali kiandaliwe mazingira mazuri ya ufanyaji kazi kwa kufuatana na misingi iliyopo kwenye mkataba wa Paris ambao unatoa zingatia kuwepo kwa hali ya uhuru bila kuingiliwa na mammlaka nyingine yoyote.