Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mpango kuwasaidia Wasri Lanka Kaskazini wazinduliwa

Mpango kuwasaidia Wasri Lanka Kaskazini wazinduliwa

Serikali ya Sri Lanka kwa ushirikiano na Umoja wa Mataifa na mashirika mengine ya kibinadamu kwa pamoja wamezindua mpango wa kuwasaidia watu wa kaskazini mwa nchi hiyo kujenga upya maisha yao.

Mpango huo wa mwaka mmoja umebuniwa ili kupata suluhu la muda mrefu yakiwemo masuala ya ujenzi wa makaazi, kusaidia katika kilimo na katika usalama wa chakula.

Mpango huo pia unahusisha jitihada kama vile kuimarisha sekta za afya, kuomdoa mabomu ya ardhini ili kutoa fursa kwa watu kurejea makwao pamoja na masuala ya elimu. Mratibu wa masuala ya kibinadamu wa Umoja wa Mataifa Neil Buhne anasema kuwa lengo kuu la mpango huu ni kupatikana kwa maendeleo ya muda mrefu kwa muda mfupi.