Kituo cha uhamiaji kufunguliwa nchini Djibouti:IOM
Katibu katika shirika la kimataifa la uhamiaji IOM William Lacy Swing yuko nchini Djibouti kwa mikutano na maafisa wa ngazi za juu serikalini kujadili njia za kushughulia suala la mahitaji ya kibinadamu kwa wahamiaji , wakimbizi na kwa watafuta hifadhi kutoka upembe wa Afrika wanaolekea nchini Yemen wakipitia ghuba ya Aden.
Lacy Swing anasema kuwa kituo cha kuwahudumia wahamiaji chini ya ufadhili wa serikali ya Japan kitafunguliwa katika mji wa Obock nchini Djibouti. Kituo hicho kitatumika kutoa usaidizi wa kibinadamu kwa wahamiaji , wakimbizi na watafuta hifadhi ambao kwa sasa wanaishi kwenye mazingira mabaya ndani na nje ya mji wa Obock.
Mwaka uliopita zaidi ya watu 30,000 walitumia mashua za wafanya magendo katika eneo la Obock wakiwemo wanawake na watoto ambapo wengi walipitia hali ngumu mikononi mwa wafanya magendo baada ya kupigwa, kubakwa na na hata kutupwa baharini.