UNHCR yakaribisha sheria mpya ya wakimbizi Mexico

28 Januari 2011

Shirika la Umoja wa Mataifa linalohudumia wakimbizi UNHCR limekaribisha hatua iliyochukuliwa na serikali ya Mexico kupitisha sheria mpya inayowalinda wakimbizi pamoja na wale wanaoomba hifadhi.

Sheria hiyo mpya ambayo imesainiwa wiki hii na Rais Felipe Calderón tayari imeanza kufanya kazi hatua ambayo imepongezwa kutokana na nchi hiyo licha kusaini mikataba ya kimataifa lakini kwa miaka mingi ilikosa sheria mahsusi juu ya wakimbizi.

Kupitia sheria hiyo wakimbizi walioko nchini humo wanapata fursa ya kufanya kazi, kufikiwa na huduma za kiafya pamoja na fursa ya kupata elimu. 

Mexico imekuwa kimbilia kubwa la wakimbizi wengi kutoka nchi za Latin American ikiwemo Colombia, Haiti, El Salvador, Honduras na Guatemala. Pia wakimbizi kutoka nchi za DR Congo, Sri Lanka, Iraq, Iran, Nepal na Nigeria wanatajwa kuingia nchi humo.

 

♦ Kutembelea ukurasa maalum wa COP26 bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter