Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

FAO kuendelea kufadhili kilimo Haiti

FAO kuendelea kufadhili kilimo Haiti

Shirika la kililo na mazao la Umoja wa Mataifa FAO linasema kuwa ufadhili katika sekta ya kilimo nchini Haiti ndio utasaidia kuwepo kwa maendeleo na pia nchi kuwa tayari kwa majanga ya kiasili ya baadaye.

Mwaka mmoja baada ya kushuhudiwa kwa tetemeko kubwa la ardhi nchini Haiti athari za tetemeko hilo bado zinaendelea kushuhudiwa sehemu za vijijini na kuchochewa zaidi na mlipuko wa ugonjwa wa kipindupindu pamoja na maporomoko ya udongo yaliyosababishwa na kimbunga Tomas na kuathiri vibaya sekta ya kilimo.

Mratibu wa shirika la FAO nchini Haiti Etienne Peterschmitt amesema kuwa jamii zinazotegemea kilimo huwa zinaathirika vibaya kutokana na majanga ya kiasili. Tangu kutokea kwa tetemeko kubwa la ardhi nchini Haiti FAO na washika dau wengine wakishirikiana na wizara ya kilimo wametoa msaada kwa familia 560 au takriban watu milioni tatu.

FAO imesambaza tani 2200 za mbegu , na tani 164 za mbolea na vifaa 190,000 za kilimo kwa wakulima nchini Haiti.