Wachezi nyota wa cricket waunga mkono vita vya ukimwi

Wachezi nyota wa cricket waunga mkono vita vya ukimwi

Wachezaji nyota wa mchezo wa cricket Virender Sehwag kutoka India na captain wa timu ya taifa ya Sri Lanka Kumar Sangakkara wameunga mkono kampeni za Umoja wa Mataifa za kukabiliana na ugonjwa wa UKIMWI kwa kuvaana dimbani.

Hatua hiyo ni sehemu ya kombe la dunia mchezo wa Cricket ambayo inafanyika kwa ushirikiano wa shirika la Umoja wa Mataifa la kukabili ugonjwa wa UKIMWI UNAIDS, na lile linalohusika na watoto UNICEF. Wachezaji hao wanahamasisha ujumbe maalumu wa kujikinga na maambukizi ya virusi vya ugonjwa huo.

Kampeni hiyo inashabaya ya kuwafikia vijana wengi zaidi kwa wakati mmoja huku wakipatiwa taarifa mbalimbali za namna ya kujiepusha na maambukizi. Pamoja na kwamba kumekuwa na taarifa za kuridhisha juu ya maambukuzi ya virusi vya ugonjwa huo ambapo kati ya mwaka 2001 hadi 2009 maambukizi yalipungua kwa asilimia 20,lakini idadi ya watu waliopata maambukizi hayo kwa kila siku mwaka uliopita ilifikia 7,000 na kila mtu mmoja kati ya hao alikuwa kijana mwenye umri kati ya miaka 15 hadi 24.