Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mwanaharakati wa ukimwi Elizabeth taylor afariki dunia

Mwanaharakati wa ukimwi Elizabeth taylor afariki dunia

Elizabeth Taylor , mwanaharakati wa vita dhidi ya ukimwi na mcheza sinema mashuhuri wa Hollywood amefariki dunia hii leo kwa matatizo ya moyo akiwa na umri wa miaka 79.

Bi Taylor amekuwa katika makao makuu ya Umoja wa mataifa mara kadhaa kuzungumzia mahitaji ya ufadhili katika utafiti na tiba ya ukimwi, pia amesafiri katika nchi za Afrika na nyinginezo zilizoathirika sana na ukimwi katika juhudi za kuleta mabadiliko.

Taylor aliwahi kuwa mwenyekiti mwanzilishi wa shirika la kimataifa la utafiti wa ukimwi liitwalo American Foundation for AIDS Reseach (AMFAR) Mwaka 1991 alianzisha mfuko maalumu "Elizabeth Taylor AIDS Foundation" ili kuchangisha fedha na kutoa huduma kwa watu wenye virusi vya HIV.

Desemba 1996 alipokea tuzo ya AMFAR kwa kazi zake za kujitolea kwenye siku ya kimataifa ya ukimwi kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa hapa New york.