Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNAIDS na IOM kukabili ukimwi kwa wahamiaji

UNAIDS na IOM kukabili ukimwi kwa wahamiaji

Mashirika ya Umoja wa Mataifa lile linalohusika na UKIMWI UNAIDS na lile la uhamiaji IOM yametiliana saini mpango wa mashirikiano ili kukabiliana na tatizo la ukimwi linalowakabili wahamiaji wengi.

Chini ya mpango huo pande zote mbili zimeazimia kuunganisha nguvu ambayo itawawezesha wahamiaji wa ndani na wale wa kimataifa wanafikia wa huduma za afya pamoja na kutobaguliwa kwa hali yoyote ile.

Michel Sidibé ambaye ni Mkurugenzi Mtendaji wa UNAIDS amesema kuwa serikali pamoja na wahisani wengi wanakila sababu kuhakikisha kwamba makundi ya watu wahamiaji wanafikiwa na huduma za kiafya ikiwemo pia kupata huduma za HIV

Mpango huo mpya pamoja na mambo mengine lakini unakusudia kuongeza uzito juu ya kulindwa kwa wahamiaji kutotumbukia kwenye maambukizi ya HIV