UM washangazwa na dhuluma dhidi ya watoto Ivory Coast

26 Januari 2011

Mjumbe maalum wa katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa katika masuala ya watoto na mizozo ameelezea kushangazwa kwake kufuatia kuendelea kwa ghasia nchini Ivory Coast yakiwemo madai ya mauaji , kuwalemaza na utekaji nyara wa watoto tangu kuanza kwa mzozo nchini humo.

Radhika Coomaraswamy pia amesema kuwa imekuwa vigumu kudhibitisha madai hayo kutokana na ugumu iliopo wa kuyafikia maneo walipo wakimbizi. Mjumbe huyo amesema kuwa wavulana wakiwemo wasichana walio idadi kubwa ya wakimbizi wanakimblia Liberia wako kwenye hatari ya kukabiliwa na dhuluma kama hizo .

Ivory Coast imekabiliwa na mzozo ulioibuka baada ya rais Laurent Gbagbo kukataa kung'atuka mamlakani hata baada ya mpinzani wake na kiongozi wa upinzani Alassane Ouattara kutambuliwa kimataifa kama mshindi kwenye uchaguzi mkuu.

 

♦ Kutembelea ukurasa maalum wa COP26 bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter