Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Miundombinu ni kikwazo cha kuwafikia wakimbizi Liberia:UNICEF

Miundombinu ni kikwazo cha kuwafikia wakimbizi Liberia:UNICEF

Shirika la kuwahudumia watoto la Umoja wa Mataifa UNICEF linasema kuwa asilimia 85 ya wakimbizi wanaoingia nchini Liberia kutoka Ivory Coast ni watoto na wanawake.

Hadi sasa zaidi ya wakimbizi 29,000 waliosajiliwa asilimia 65 kati yao ni watoto , asilimia 50 wakiwa ni wanawake huku wanaume wakiwa chini ya asilimia 15.

Inaripotiwa kuwa ikiwa hali hii itaendelea idadi ya wakimbizi wanaoingia nchini Liberia itafikia wakimbizi 100,000 ifikapo mwishoni mwa mwezi Aprili. Wakimbizi hao wamepiga kambi kwenye vijiji 32 wakati vijiji wanamoishi vikitajwa kuwa moja ya sehemu maskini zaidi nchini Liberia.

Hali mbaya ya barabara na madaraja vitatatiza usafiri kwenda kwa maeneo waliko wakimbizi na kuna hofu kuwa iwapo hatua za dharura hazitachukuliwa maeneo hayo huenda yasifikike kabisa utakapowadia msimu wa mvua mwezi Aprili.