UM una jukumu la kukemea uvunjaji wa haki za binadamu:Ban

24 Januari 2011

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amesema kuwa Umoja huo ndiyo wenye dhamana ya kukemea na kuzungumzia hadharani vitendo vyovyote vya uvunjivu wa haki za binadamu na kuwapa sauti wale wanaoonewa.

Ban amesema kuwa shabaya ya kuasisiwa kwa Umoja wa Mataifa ambayo ilikuja kufutia kuzuka kwa vita ya pili ya dunia ilikuwa ni kuhakikisha kwamba dunia haitumbukii tena kwenye matatizo ya vita hivyo Umoja huo unaendelea kusalia na jukumu lake la kuhakikisha kwamba inakuwa mstari wa mbele kuwasemea wanyonge.

Katibu huyo ambaye alikuwa akizungumza kwenye kanisa moja linalofahamika kama Manhattan's Park East Synagogue kama sehemu ya mkesha kuelekea kwenye kuadhimisha mauwaji ya Holocaust amesisitza haja ya kuungwa mkono Umoja huo wa Mataifa ili uweze kutimiza shabaya yake.

Baraza la usalama la Umoja wa Mataifa liliipitisha January 27 kila mwaka kama siku ya kuadhimisha mauwaji ya Holucaust .

 

♦ Kutembelea ukurasa maalum wa COP26 bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter