Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Soko la chakula kisichofaa kwa watoto lipunguzwe:WHO

Soko la chakula kisichofaa kwa watoto lipunguzwe:WHO

Shirika la afya duniani WHO limesema watoto kote duniani wamekuwa wahanga wa masoko ya vyakula vilivyonona mafuta, vyenye kiwango kikubwa cha sukari au chumvi ambavyo vinaongeza hatari ya kizazi hicho kupata magonjwa yasiyo ya kuambukiza wakati wa maisha yao.

WHO inazitaka nchi kuchukua hatua kupunguza hali hiyo kwa kutekeleza hatua za kimataifa zilizoidhinisha. Kwa mujibu wa tathimini ya kupata ushahidi wa hali hiyo matangazo ya televisheni, yanalaumiwa kwa kiasi kikubwa kwa kuchagiza soko la vyakula visivyofaa kwa afya za watoto, kuwahamasisha chakula gani wale, kuwafanya waagize chakula hicho na ,tabia ya kupendelea kula vyakula hivyo.

Mai 2010, nchi wanachama wa WHO waliidhinisha mapendekezo mapya ya jinsi ya kutangaza masoko ya vyakula na bidhaa zisizo kilevi kwa ajili ya watoto. Mapendelezo hayo yanataka kuchukuliwe hatua za kitaifa na kimataifa kupunguza kiwango cha watoto kupata fursa ya matangazo ya masoko ya vyakula hivyo na kupunguza matumizi ya mbinu zenye ushawishi mkubwa kwa kutangaza vyakula hivyo kwa watoto.

Mkurugenzi mkuu wa magonjwa yasiyo ya kuambukiza na afya ya akili kwenye WHO Dr Ala Alwan anasema magonjwa kama ya moyo, saratani na kisukari leo ni tishio kubwa kwa afya za bianadamu na maendeleo ya kiuchumi na kijamii.

Lakini amesema kwa kutekeleza mapendekezo haya kutasaidia kwa kiasi kikubwa juhudi za kuzuia vyakula visivyofaa kwa afya ambavyo huchangia kwa kiasi kikubwa maradhi haya. Takwimu za WHO zinaonyesha kwamba watoto milioni 43 walio chekechea duniani kote wana maradhi ya unene au wanauzito wa kupita kiasi . Na tathimini ya kisayansi imedhihirisha kwamba matangazo ya televisheni ymemechakia kiasi cha matatatizo hayo.