Matatizo ya kiuchumi Ireland yamesababisha kukiukwa haki za binadamu:UM

21 Januari 2011

Hali mbaya ya kiuchumi na kifedha inayoiandama Ireland inazalisha kitisho kikubwa kwa makundi ya watu waliopembezoni ambayo hata hivyo yanafaidika kidogo na chipuo jipya la uchumi linalojitokeza kwa nchi hiyo.

Kwa mujibu wa mtaalamu wa Umoja wa Mataifa anayehusika na masuala ya umaskini Magdalena Sepúlveda hata hivyo amekaribisha hatua zilizochukuliwa miongo kadhaa ili kukabili athari mbaya zilisababishwa na kuanguka kwa uchumi, lakini amesema kuwa bado hatua hizo hazijatoa majibu sahihi kwa baadhi ya makundi ya watu.

Amesema kwa mfano kwenye eneo la hifadhi ya jamii bado inasua sua hataua ambayo inakaribisha janga la kijamii. Ametaka kuwepo kwa zingatio kubwa wakati wa kushulikia maanguko ya kiuchumi kwani uzoefu unaonyesha kwamba mahitaji yanayofungamana na haki za binadamu yanapuzwa mara kwa mara.

 

♦ Kutembelea ukurasa maalum wa COP26 bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter