Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Elimu ya msingi kwa wote Burundi inapiga hatua lakini bado kuna changamoto

Elimu ya msingi kwa wote Burundi inapiga hatua lakini bado kuna changamoto

Wahenga walinena elimu ni ufunguo wa maisha bila elimu maendeleo ya kiuchumi, kisiasa na kijamii yatakuwa ndoto.

Na kwa kulitambua hilo wakuu wan chi waliokutana kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa mwaka 2000 waliainisha malengo manane ya maendeleo ya milenia na mojawapo ni hilo la elimu. Miaka mine tuu imesalia kabla ya 2015 muda wa kutimiza malengo hayo.

Na moja ya hatua muhimu ni kutoa elimu ya msingi bure kwa wote, Burundi inafanya jivyo jambo ambalo limechagia sana katika juhudi za kutaka kutimiza lengo hilo la milenia.Takwimu mpya zaonyesha kwamba watoto wa umri unaostahili wamekwenda shule kwa asilimia 94 hivi sasa wanasoma nchini Burundi.

Lakini changamoto kubwa bado ni viwango na mazingiza ya jumla ya elimu bora kama anavotufahamisha muandishi wetu wa Bujumbura Ramadhani KIBUGA katika makala hii.

(PKG BY RAMADHAN KIBUGA)