UM walaani mashambulizi ya kigaidi nchini Iraq
Mjumbe maalumu wa Umoja nchini Iraq amelaani vikali vitendo vya kigadi vinavyowalenga askari wanaopatiwa mafunzo katika mji wa Tikrit ambako watu kadhaa wameuwawa na wengine kujeruhiwa.
Katika taarifa yake aliyoitoa hii leo Ad Melkert ameelezea masikito yake na kusema kwamba makundi hayo ya kigadi yanaweka shabaya yao kwa askari ambao wamechukua jukumu la kutaka kulijenga upya taifa hilo. Ametuma salam za rambi rambi kwa ndugu na jamaa waliofikwa na msiba huo na kuwaombea dua wapone haraka wale wote waliojeruhiwa.
Vikosi vya usaidizi vya Umoja wa Mataifa nchini Iraq (UNAMI) vimekuwa vikielezea hali ya wasiwasi inayoikumba nchi hiyo kutokana na mashambulizi ya mara kwa mara yanayoibuka.