Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Bei kubwa ya kasumba kuvuruga vita dhidi ya zao hilo:UNODC

Bei kubwa ya kasumba kuvuruga vita dhidi ya zao hilo:UNODC

Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya uhalifu na madawa UNODC imeonya kwamba ongezeko la bei ya kasumu linaweza kuwashawishi wakulima wengi kurejea katika uzalishaji wa zao hilo.

Onyo hilo limetolewa leo katika ripoti ya 2010 baada ya utafiti wa kina wa uzalishaji wa kasumba nchini Afghanistan.

Ongezeko la bei limetokana na tetesi kwamba uzalishaji ulipungua kwa nusu mwaka 2010 na operesheni za kijeshi zinazoendelea nchini humo na kuwafanya wakulima wengi kuwa na sintofahamu ya hatima ya uzalishaji wa zao hilo. George Njogopa anaarifu.

(SAUTI YA GEORGE NJOGOPA)