Skip to main content

UNESCO yalaani mauji ya wandishi wa Kifaransa Tuniasia

UNESCO yalaani mauji ya wandishi wa Kifaransa Tuniasia

Mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na uteteaji wa uhuru wa vyombo vya habari, amelaani vikali tukio la kuuwawa kwa mwandishi mmoja wa habari raia wa Ufaransa huko Tunisia ambaye aliuwawa wakati akifuatilia maandamano yaliyokuwa yakifanyika nchini humo.

Mwandishi huyo wa habari Lucas Mebrouk Dolega anayefanya kazi ya upigaji picha na shirika moja la European Press Agency alifariki dunia hapo jumatatu kutokana na majeraha makali aliyoyapata baada ya kupigwa vibaya na mabomu ya machozi wakati akifuatilia maandamano yaliyoshuhudia rais Zine El Abidine Ben Ali akiikimbia nchi yake.

Katika taarifa yake juu ya tukio hilo, Mkurugenzi Mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na masuala ya elimu,sayansi na utamaduni (UNESCO) Irina Bokova amesema kuwa kifo cha mwandishi huyo kinakumbusha mazingira magumu na ya hatari ambayo daima wanaandishi wa habari hukupamba nayo.

Ametolea mwito mamlaka zinazohusika kuongeza bidii ili kuhakikisha kwamba waandishi wa habari duniani kote wanafanya kazi zao kwenye mazingira salama na ya uhakika. Wananchi wa Tunisa walifurika bara barani wakishinikiza kuondolewa madarakani kwa utawala wa Zine El Abidine Ben Ali, kutokana na kuongezeka kwa ughali wa maisha pamoja na kushamiri wa kitendo vya dhulma na rushwa.