Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Uchumi unatarajiwa kukuwa kwa wastan 2011 na 2012

Uchumi unatarajiwa kukuwa kwa wastan 2011 na 2012

Uchumi wa dunia unatarajiwa kukua kwa kiwango cha wastani cha kati ya asilimia 3 na 3.5 kwa 2011 na 2012, kwa mujibu wa ripoti mpya ya Umoja wa Mataifa.

Ripoti hiyo ya hali ya uchumi wa dunia na matarajio kwa mwaka 2011 iliyotolewa leo mjini Geneva inatabiri kwamba uchumi utakuwa kwa kiwango kikubwa katika nchi zinazoendelea.

Alfredo Calcagno mwanauchumi katika mkutano wa Umoja wa Mataifa wa biashara na maendeleo anasema ukuaji huu wa asilimia 3 au 3.5 utatoka kwa nchi zinazoendelea a kwani kwingineko asilimia mbili, huku uchumi unaochipukia utakuwa kwa asilimia 4 na nchi zinazoendelea utakua kwa asilimia 6. Amesema pia kutakuwe na tofauti ya viwango vya ukuaji katika mabara duniani.