Skip to main content

Kurejea kwa Baby Doc Haiti kwaweza kumtia matatani:UM

Kurejea kwa Baby Doc Haiti kwaweza kumtia matatani:UM

Mashitaka ya ukiukaji wa haki za binadamu ynaweza kuwasilishwa dhidi ya Rais wa zamani wa Haiti Jean-Claude Duvalier ambaye pia anafahamika kama Baby Doc, kwa mujibu wa mkuu wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa.

Bwana Duvalier amerejea Haiti Jumatatu wiki hii baada ya kuishi uhamishoni nchini Ufaransa kwa miaka 25. Utawala wake wa miaka 15 ulighubikwa na ukiukaji mkubwa wa haki za binadamu dhidi ya watu wa Haiti. Rupert Colville ni msemaji wa kamishna mkuu wa haki za binadamu.

(SAUTI YA RUPERT COLVILLE)