Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Muafaka wa Sudan Kusini na Kaskazini kuhusu Abyei wakaribishwa:UNMIS

Muafaka wa Sudan Kusini na Kaskazini kuhusu Abyei wakaribishwa:UNMIS

Mpango wa Umoja wa Mataifa nchini Sudan UNMIS umekaribisha muafaka uliofikiwa baina ya Sudan Kaskazini na Kusini tarehe 17 mwezi huu mjini Kadugli kuhusu usalama wa jimbo la Abyei.

Majadiliano yao kushu suala hilo yaliongozwa na waziri wa mambo ya ndani wa Sudan Kaskazini Ibrahim Mohamed Hamid na waziri wa mambo ya ndani wa Sudan Kusini Gier Chuang Aluong.

Masuala muhimu ya muafaka huu ni pamoja na kutoa usalama wa jimbo la Abyei kwa kupeleka vikosi vya pamoja ili kuhakikisha uhuru wa jamii ya Misseriya ambao ni wafugaji kuingia Abyei na maeneo ya Kusini, na kutoa usalama kwa wakimbizi wa ndani kurejea nyumbani.

Makubaliano hayo kutokana na muafaka ulioafikiwa wiki jana baina ya jamii za Misseriya na Dinka Ngok kwenye jimbo hilo. UNMIS imezipongeza pande hizo mbili kwa kuendelea na juhudi za kutatua tofauti zao kwa njia ya amani na majadiliano, na imesema iko tayari kutoa msaada wowote muhimu utakaohitajika.