Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mashitaka dhidi ya mauaji ya Hariri yawsilishwa rasmi

Mashitaka dhidi ya mauaji ya Hariri yawsilishwa rasmi

Mwendesha mashitaka mkuu wa mahakama maalumu ya Lebanon Daniel Bellemare amewasilisha mashitaka rasmi ya washukiwa wa mauji ya aliyekuwa waziri mkuu wa Lebanon Rafiq Hariri.

Bwana Bellemare amesema kuwasilisha mashitaka hayo ni hatua muhimu kwa watu wa Lebanon, jumuiya ya kimataifa na wote wanaoamini haki ya kimataifa.

(SAUTI YA DANIEL BELLEMARE)

Hata hivyo majina ya washukiwa hao hayatajulikana kwa wiki kadhaa, Bellemare amewasilisha majina na vielelezo kwa jaji Daniel Fransen ambaye sasa atapitia kabla ya hatua inayofuata kufanyika.

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon ameelezea kuunga mkono kwa mahakama hiyo maalumu.