Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Israel yaenendelea kukiuka sheria Ukingo wa Magharibi: UM

Israel yaenendelea kukiuka sheria Ukingo wa Magharibi: UM

Mjumbe maalum wa Umoja wa Mataifa Richard Falk ameelezea hisia zake na kuvitaja kama ukiukaji wa sheria vitendo vya Israel kwenye ardhi inayoikalia kwenye ukingo wa magharibi vikiwemo vya mauaji ya wapalestina wanne wiki mbili zilizopita.

Mauaji yaliyotekelezwa na wanajeshi wa Israel na ubomoaji wa hoteli ya kihistoria mashariki mwa mji wa Jerusalem ili kutoa nafasi kwa ujenzi wa makazi zaidi ya walowezi wa kiyahudi. Mjumbe huyo amesema kuwa vitendo hivyo vyote vya kuendelea kuikalia ardhi ya wapalestina pamoja na matumizi ya nguzu kupita kiasi na Israel dhidi ya wapalestina havikubaliki .George Njogopa anaripoti.

(SAUTI YA GEORGE NJOGOPA)