Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UM kuchunguza mauaji ya watu nchini Tunisia

UM kuchunguza mauaji ya watu nchini Tunisia

Tume ya kutetea hali za binadamu ya Umoja wa Mataifa inasema kuwa iko tayari kushiriki kwenye uchunguzi kuhusiana na mauaji yanayokisiwa kufanyika nchini Tunisia wakati wa maaandamano juma hili.

Hapo jana tume hiyo iliitaka serikali ya Tunisia kuhakikikisha kuwa wanajeshi wake hawatumii nguvu kupita kiasi dhidi ya waandamanajina na kuendesha uchunguzi ulio wazi kuhusiana na mauaji wakati wa maandamano ya hivi majuzi ya kipinga kupanda kwa bei ya vyakula, Uhaba va nafasi za ajira , ufisadi na ukiukaji wa haki za binadamu.