Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Uchumi na uwekezaji Afrika kukua 2011:IMF

Uchumi na uwekezaji Afrika kukua 2011:IMF

Bara la afrika linatazamiwa kuwa na ustawi mzuri wa kibiashara mwaka huu wa 2011, hali ambayo imechangiwa na mafanikio iliyopata wakati dunia ulioshuhudiwa mwamo wa kiuchumi.

Shirika la fedha la kimataifa katika taarifa yake imesema kiwango cha uwekezaji wa nje barani afrika kinatazamiwa kuongezeka na hivyo kuwa shabaya ya masoko mengi ya kimataifa. China iliyomshirika mkubwa wa afrika inatazamiwa kuimarisha mahusiano yake na huenda pande zote mbili zikashuhudia mahitajiano ya kibiashara yakiongezeka.

Hata hivyo IMF imeonya kuwa nchi za afrika zitapaswa kufanyia marekebisho makubwa baadhi ya sera zake zinazohusika na uchumi na uwekezaji wa nje.