Skip to main content

Ban ayataka maifa ya G-77 kuusaidia UM kutekeleza wajibu

Ban ayataka maifa ya G-77 kuusaidia UM kutekeleza wajibu

Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amelitaka kundi la nchi zinazoendelea lijulikanalo kama "kundi la 77" na China kuweka sauti zao na kuusadia Umoja wa Mataifa kutimiza malengo yake.

Malengo hayo ni pamoja na vita dhidi ya umaskini na kupambana na mabadiliko ya hali ya hewa yakiwemo pia masuala ya kuwainua wanawake. Akiongea kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa wakati wa sherehe za kuikabidhi Argentina uenyekiti wa kundi la G77 kutoka Yemen, Ban amesema kuwa huu ni wakati wa kushuhudiwa mabadiliko.

Kundi hilo la nchi 77 lililobuniwa mwaka 1964 kwa sasa lina wanachaama zaidi ya 130 ikiwemo China. Kundi hilo linatoa fursa kwa kutaka nchi za kusini kushirikina kutoa maoni yao kuhusu masuala ya uchumi kwenye Umoja wa Mataifa.

Ban amesema kuwa jitihada za kukabiliana na mabadiliko ya hali ya hewa lazima zipewe kipaumbele mwaka huu wa 2011 kwa kutoa usaidizi kwa nchi zinazoendelea na pia jitihada za kuzuia uhaaribifu wa misitu.