Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Maelfu ya watu wasambaratishwa na mafuriko Sri Lanka: UM

Maelfu ya watu wasambaratishwa na mafuriko Sri Lanka: UM

Watu karibu milioni moja wamesambaratishwa na mafuriko Katikati na Mashariki mwa Sri Lanka yamesema mashirika ya misaada ya Umoja wa Mataifa.

Duru za habari kutoka nchini humo zinasema katika maeneo mengine maji ya mafuriko hayo yanafikia mita mbili na kina kinaendelea kuongezeka. Watu 18 wamearifiwa kufa hadi sasa. Lin Sambili na taarifa kamili.

(SAUTI YA LIN SAMBILI)