Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ban ataka kuwe na utulivu na mazungumzo Tunisia

Ban ataka kuwe na utulivu na mazungumzo Tunisia

Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki moon ametaka kuwe na utulivu nchini Tunisia baada ya kushuhudiwa kwa mapigano kati ya wanajeshi na waandamanaji ambapo karibu watu 14 wameuawa siku chache zilizopita.

Kwa mujibu wa vyombo vya habari serikali ya Tunisia imeamrisha kufungwa kwa mashule na taasi zingine za elimu ya juu kutokana na kuendelea kushuhudiwa kwa ghasia zinazokisiwa kusababishwa na mifumo mibaya ya ajira na viongozi wa nchi. Ban amezitaka pande husika kutatua tofauti zao kwa njia ya mazungumzo na kutaka kuwe na haki ya kusema.