Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UM waitaka serikali ya DRC kuchunguza madai ya ubakaji

UM waitaka serikali ya DRC kuchunguza madai ya ubakaji

Ujumbe wa Umoja wa Mataifa unaopambana na dhuluma za kimapenzi kwenye sehemu zilizo na mizozo umetoa wito kwa serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo kuchunguza mara moja ripoti kuwa kumekuwa na ubakaji katika siku za hivi majuzi kwenye mkoa wa maashariki wa Kivu Kusini.

Mapema juma hili shirika la Medecins Sans Frontieres (MSF) liliripoti kuwa wanaume waliokuwa wamejihami waliwabaka zaidi na wanawake 30 mnamo tarehe mosi mwezi huu kwenye mji wa Fizi ulio mashariki mwa nchi. Lin Sambili na taarifa kamili.

(SAUTI YA LIN SAMBILI)