Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UM waelezea hofu yake kuhusu ghasia na uchochezi nchini Ivory Coast

UM waelezea hofu yake kuhusu ghasia na uchochezi nchini Ivory Coast

Maafisa wawili wa Umoja wa Mataifa leo wameelezea hofu yao juu ya hali nchini Ivory Coast , na kusema baadhi ya viongozi wanachagiza ghasia na chuki miongoni mwa jamii na kuonya kwamba wanaohusiaka watawajibishwa chini ya sheria za kimataifa.

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon wakati huohuo ameonya juu ya jaribio la kutaka kushambulia hotel ya Golf ambako Rais aliyechaguliwa Alassane Ouattara na wapambe wake wameweka makao na ambako panalindwa na wanajeshi ya umoja wa Mastaifa nchini humo UNOCI.

Nao Francis Deng mshauri maalumu wa Katibu Mkuu katika kuzuaia mauaji ya kimbari na Edward Luck mshauri katika masuala ya kuwalinda raia wamesema kunaendelea kuwepo ripoti ambazo hazijathibitishwa za ukiukaji mkubwa wa haki za binadamu unaofanywa na wafuasi wa Rais Laurent Gbagbo na jeshi la nchi hiyo ambalo lipo chini yake.

Pia wamesema kuna matumizi ya lugha za uchochezi na uchagizaji wa chuki na ghasia. Bwana Deg ameongeza kuwa taarifa za madai kwamba nyumba za wafuasi wa upinzani kwenye mji wa Abijan Magharibi mwa nchi kuwa zimewekwa alama kuonyesha makabila yao ni za kutia hofu.