Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wakimbizi wanawake Iraq wanakabiliwa na changamoto: IOM

Wakimbizi wanawake Iraq wanakabiliwa na changamoto: IOM

Shirika la kimataifa la uhamiaji IOM limesema upungufu wa chakula, ukosefu wa ajira na huduma za afya ni changamoto kubwa inayowakabili wanawake wa Iraq ambao ni wakimbizi wanaorejea nyumbani na kuwa na jukumu la kuangalia familia zao.

Katika utafiti wa karibuni uliofanywa na IOM na kuwalenga wanawake ambao ndio walezi wa familia umebaini kuwa familia 1355 kati ya wakimbizi waliorejea zinaongozwa na kusimamiwa na wanawake.

Hata hivyo asilimia 74 ya familia hizo zinakabiliwa na changamoto kubwa za kupata mahitaji muhimu kama chakula, huduma za afya na mambo mengine muhimu, kwa sababu ama wanawake hao hawawezi kufanya kazi, au hawawezi kupata ajira kutokana na matatizo ya kiafya au mila. Liana Paris ni afisa wa operesheni za IOM mjini Baghdad.

(SAUTI YA LIANA PARIS)