Saudi Arabia isitishe kuwarejesha kwa nguvu wakimbizi wa Somalia: UNHCR

23 Disemba 2010

Shirika la kimataifa la kupigania haki za binadamu Human Rights watch leo limesema serikali ya Saudi Arabia ni lazima isitishe mara moja kuwarejesha kwa nguvu mjini Mogadishu wakimbizi wa Somalia na waomba hifadhi.

Kauli hiyo inunga mkono taarifa iliyotolewa hivi karibuni na shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR. Duru za habari zinasema serikali ya Saudia imewarejesha kwa nguvu takribani Wasomali 150 hadi mjini Moghadishu Desemba 17 mwaka huu ,wengi wakiwa ni watoto kutoka mjini Jeddah.

UNHCR inasema kwa mwezi wa Juni na Julai Saudia iliwarejesha Wasomali wapatao 2000. Jason Nyakundi anaripoti.

(SAUTI YA JASON NYAKUNDI)

 

♦ Kupata takwimu za waathirika vitani Ukraine bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter