Idadi ya waliokufa, kujeruhiwa na kupotea inaongezeka Ivory Coast : UNOCI
Wakati huohuo taarifa iliyotolewa leo mjini Abijan na mpango wa Umoja wa Mataifa nchini Ivory Coast UNOCI inasema idadi ya waliokufa, kujeruhiwa na watu wasiojulikana waliko inaongezeka kwa kasi.
Taarifa hiyo imeongeza kwamba njia zote za kuingia na kutoka hotel ya Golf inayotumiwa na Alassane Ouattara zimefungwa na wanajeshi wa kambi ya Bwana Laurent Gbagbo wanaoungwa mkono na makundi ya vijana ambao wamevalia vinyago na kuwa na silaha na maroketi kama anavyofafanua mwakilishi wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa nchini humo Y.J.Choi ambaye pia ni mkuu wa UNOCI
(SAUTI YA Y.J.CHOI)
Ameongeza kuwa UNOCI itaendelea kutumia uwezo wake kufanya kila liwezekanalo kuhakikisha ulinzi kwa raia huku ikiweka nyaraka za ukweli mambo ili kusaidia vyombo husika kuchukua hatua za kuwawajibisha wanaohusika na machafuko.