Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Sudan lazima muafikiane kuhusu jimbo la Abyei:UM

Sudan lazima muafikiane kuhusu jimbo la Abyei:UM

Serikali za Sudan na Sudan Kusini zimetakiwa na baraza la usalama la Umoja wa Mataifa kufikia muafaka kuhusu mvutano wa jimbi lenye utajiri wa mafuta la Abyei.

Chini ya makubaliano ya amani ya CPA ya mwaka 2005 yaliyomaliza zaidi ya muongo wa vita katika ya Sudan Kusini na Kaskazini, kura ya maoni itafanyika Januari mwakani kwa watu wa Abyei kuchagua endapo wawe sehemu ya Kaskazini ama Kusini mwa Sudan.Na kura nyingine ya maoni itaruhusu Sudan Kusini kuamua endapo iwe taifa huru ama la.

Rais wa baraza la usalama mwezi huu balozi wa Marekani kwenye Umoja wa Mataifa Susan Rice amesema limekaribisha hatua ya kukamilisha uandikishaji wapiga kura Sudan Kusini lakini inahofia kutofikiwa muafaka kuhusu jimbo la Abyei.

Amesema baraza linazitaka pande husika kutuliza mvutano Abyei,na kufikia makubaliano haraka kuhusu jimbo hilo na masuala mengine yaliyo kwenye mkataba wa CPA, na kutatua kutatua masuala ya baada ya kura ya maoni kama mpaka, usalama,uraia, madeni, mali, sarafu na mali asili.