Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mapigano makali yamezuka leo mjini Abijan Ivory Coast

Mapigano makali yamezuka leo mjini Abijan Ivory Coast

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amewaonya watu wanaochochea au kuchaguiza ghasia, au kutumia vyombo vya habari kwa lengo hilo nchini Ivory Coast kuwa watawajibishwa kwa vitendo vyao.

Ban ametoa ujumbe huo kufuatia mvutano wa kisiasa unaoendelea Ivory Coast baada ya Rais Laurent Bagbo kutoyakubali matokeo ya duru ya pili ya Urais yaliyompya ushindi Alassane Ouattara. Leo ghasia zimezuka baada ya polisi kupambana na waandamanaji mjini Abijan na duru zinasema watu wane wameuawa. Akiwsilisha ujumbe wa Katibu Mkuu memaji wa Umoja wa Mataifa Martin Nersicky amesema.

(SAUTI YA MARTIN NERSICKY)

Habari zinasema milio ya risasi ilitawala mjini Abijan, kabla ya wafuasi wa Ouatarra kuanza maandamano kuelekea kwente kituo cha televisheni cha serikali ambacho kwa sasa kimeelzwa kuzingirwaa na jeshi. Pia kumekuwa na majibishano ya risasi nje ya hoteli anayokaa bwana Ouatarra na wasaidizi wake.