Skip to main content

Duru ya pili ya chanjo polio kuhitimishwa Congo Brazzaville:UNICEF

Duru ya pili ya chanjo polio kuhitimishwa Congo Brazzaville:UNICEF

Wizara ya afya ya Congo Brazzaville, shirika la kuhudumia watoto UNICEF, shirika la afya duniani WHO na Rotary International leo watahitimisha duru ya pili ya chanjo ya polio.

Kama anavyofafanua msemaji wa UNICEF Marixie Mercado.

(SAUTI YA MERXIE MERCADO)

Ameongeza kuwa chanjo hiyo itakomesha mlipuko wa ugonjwa huo ambao tayari umeshakatili maisha ya watu 179 na kuambukiza wengine 476 tangu ulipozuka mjini Pointe Noire Oktoba mosi mwaka huu. Mambo mawili yamejitokeza kutokana na mlipuko wa ugonjwa huo Congo, kwanza miongoni mwa waliopooza na polio kwa wastani asilimia 5 hado 10 hufa mishipa inaposhindwa kufanya kazi, na pili idadi kubwa ya walioambukizwa na kufa asilimia 60 ni vijana wanawake na wanaume wa miaka kati ya 15 na 29.