Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Visa na vifo vya malaria vinapungua duniani :WHO ripoti 2010

Visa na vifo vya malaria vinapungua duniani :WHO ripoti 2010

Ripoti ya mwaka 2010 ya dunia kuhusu hali ya malaria inaonyesha kuwa hatua zimepigwa katika kufikia malengo ya kimataifa ya kutokomeza malaria.

Mipango ya kupambana na malaria kwa kutoa vyandarua vilivyo na dawa kwenye nchi zilizoathirika zaidi hasa Afrika kati ya 2008 hadi mwisho wa mwaka huu zimeokoa maisha ya watu zaidi ya milioni 500 waliokuwa katika hatari. Ripoti hiyo iliyozinduliwa leo na shirika la afya duniani WHO inasema pia kupuliza dawa majumbani kumesaidia asilimia 10 ya watu wote walio katika hatari ya kupata malaria, pia inaelezea ni jinsi gani upatikanaji wa dawa za kuzuia malaria kwa wanaozihitaji zaidi unavyozaa matunda.Dr Robert Newman kutoka WHO anasema hii ni habari njema.

(SAUTI YA DR ROBERT NEWMAN)

Ripoti hiyo inasema nchi 11 kati ya 43 za Afrika zilizo na tatizo la malaria zimearifu kupungua kwa vifo au visa vya ugonjwa huo kwa zaidi ya asilimia 50 katika muongo uliopita na nje ya Afrika nchi nyingi zinatokomeza kabisa ugonjwa huo.