Thamani ya uzalishaji wa opium Kusini Mashariki mwa Asia yaongezeka

13 Disemba 2010

Thamani ya uzalishaji wa mihadarati aiana ya opium Kusini Mashariki mwa Asia imeongezeka na kufikia dola milioni 219 kwa mujibu wa ofisi ya Umoja wa Mataifa ya madawa na uhalifu UNODC.

Ripoti iliyotolewa leo na ofisi hiyo ikiyaguma mataifa ya Laos, Myanmar na Thailand inasema hili ni ongezeko la dola milioni 100 zaidi ya makadirio ya mwaka 2009.

UNODC imetaja kwamba Myanmar insehemu kubwa inayotumika kwa kilimo cha opium ikiwa la ekari 38,000, huko Laos ikiongeza uzalishaji kwa asilimia 58 kutoka ekari 1900 hadi ekari 3000.

Kwa Thailand wakulima wadogowadogo pia wameongeza kilimo kutoka ekari 211 hadi kufikia ekari 289.

 

♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter