Baraza la usalama la UM launga mkono ushindi wa mgombea wa upinzani Ivory Coast

9 Disemba 2010

Barasa la usalama la Umoja wa Mataifa limeunga mkono ushindi wa mgombea wa upinzani wa kiti cha urais nchini Ivory Coast Alassane Ouattara hata baada ya madai ya aliyekuwa rais wan chi hiyo Laurent Gbagbo kuwa alishinda uchaguzi huo na kuonya kuwa hatua zitachukuliwa dhidi ya yeyote ambaye atatishia usalama wa taifa hilo lililogawanyika.

"Kulinagana na ECOWAS kumtambua bwana Alassane Dramane Ouattara kama rais aliyechaguliwa wa Ivory Coast na mwakilishi wa wa sauti za watu wa Ivory Coast ilivyotangazwa na tume huru ya uchaguzi , wanachama wa baraza la usalama la UM wametoa wito kwa washikadau wote kuheshimu matokeo ya uchaguzi huo"

Kupitia ujumbe kwa vyombo ya habari baraza hilo linalaani majaribo yoyote ya kupinga uamuzi wa wapiga kura au shughuli ya uchaguzi iliyokuwa wazi . George Njogopa na taarifa kamili

 

♦ Kurambaza ukurasa mahsusi wa Siku ya Kiswahili Duniani bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter