Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ni muhimu kuzidisha mapambano dhidi ya unyanyasaji wa kijinsia wakati wa vita: Ban

Ni muhimu kuzidisha mapambano dhidi ya unyanyasaji wa kijinsia wakati wa vita: Ban

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amesema kumekuwa na ongezeko kubwa la visa vya ubakaji katika maeneo yanayokumbwa na migogoro, hivyo ametaka kuongezwa kwa nguvu ili kudhibiti vitendo hivyo na hata ikiwezekana kuwachukulia hatua kali wahusika wake.

Ameeleza kuwa licha ya kuwepo kwa juhudi mbalimbali zinazofanywa na jumuiya za kimataifa kutokomeza hali hiyo, lakini mafanikio yake yanafukiwa na kukithiri kwa vitendo vya unyanyasaji wa kinsia na ubakaji.

Ametoa wito kuimarishwa mifumo ya kisheria na kidola ili wahusika wake wafikishwe kwenye mikono ya sheria.