Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UM watoa wito wa kuwepo kwa mbinu mpya kwenye mpango wa amani wa Mashariki ya Kati

UM watoa wito wa kuwepo kwa mbinu mpya kwenye mpango wa amani wa Mashariki ya Kati

Mratibu wa mpango wa amani katika eneo la Mashariki ya Kati amesema kuwa kuendelea na unjezi wa makaazi ya walowezi wa Kiyahudi unaondeshwa na Israel katika ardhi wa Wapalestina kunahujumu mpango wa kutafuta amani katika eneo hilo.

Robert Serry amesema kuwa ujenzi wa makaazi hayo unaenda kinyume na mpango wa amani na sheria ya kimataifa na kuendelea na ujenzi huo kunavunja matumaini ya kupatikana kwa suluhu. Serry amesema kunahitajika kufanyiwa mabadiliko mbinu za mpango huo wa amani. Hata hivyo amesema kuwa ni jambo la kutia moyo kuwa Marekani imeonyesha dalili za kujitolea kuendelea na juhudu za kupatikana kwa amani Mashariki ya Kati na kuzitaka pande zinazohusika kutoa ushirikiano unaohitajika.